Posts

Showing posts from July, 2020

RIWAYA YA KISWAHILI NA TAHAKIKI

      RIWAYA YA KISWAHILI NA TAHAKIKI CHUO KIKUU CHA ARUSHA NA:  LEBABU S.S Maana ya Fasihi Dhana ya fasihi imekuwa ikijadiliwa kwa karne nyingi na wataalamu mbalimbali ulimwenguni kote. Huko Ulaya dhana hii ilikuwa ikihusishwa na vitu kadhaa. Hata Afrika neno fasihi limezua mjadala mkubwa sana kwa wanafasihi katika taaluma hii. Miongoni mwa wataalamu ambao wamechangia kuhusu maana ya fasihi ni pamoja na Sengo na Kiango (1977), Kirumbi (1975), Mazrui (1980) na wengine wengi. Kiulimwengu hasa huko Ulaya dhana ya fasihi imekuwa ikihusishwa na neno la kilatini litera likiwa na maana ya herufi au uandikaji. Hata neno la Kiingereza ‘literature’ limechipuka kutoka hapo. Mitazamo iliyotawala dhana ya fasihi ipo mitano Mtazamo wa kwanza ni ule unaodai kuwa fasihi ni tafsiri ya neno la Kiingereza Litereture ambalo asili yake ni neno la Kilatini likiwa na maana ya herufi au uandikaji. Hivyo basi mtazamo huu unaamini kuwa fasihi ni jumla ya maaandishi yote katika lugha. Wellek ...

Uchambuzi wa riwaya ya Barua Ndefu Kama Hii

Image
                                             KITIVO CHA ELIMU IDARA YA KISWAHILI JINA LA KOZI :   RIWAYA YA KISWAHILI NA TAHAKIKI  MSIMBO WA KOZI :   EDK 07402 INAWASILISHWA KWA  :  Madam. S. LEBABU INAWASILISHWA NA    :  SOMEKE B. KIBANDIKO NAMBA YA USAJILI    :  2018100202 Swali Kwa kutumia riwaya moja uliyosoma, Chambua mambo yafuatayo Uchambuzi wa fani na maudhui katika Riwaya teule Nadharia za Uchambuzi wa Riwaya Riwaya ya Kiswahili namapokeo ya kiasili Athari za Utamaduni wa nje katika Riwaya ya Kiswahili TAREHE YA KUWASILISHA 03-JULY-2020 UTANGULIZI Dhana ya Riwaya imeweza kuelezwa na wataalamu mbalimbali. Mulokozi (1996) anaeleza kuwa, Riwaya ni masimulizi marefu ya kinathari yaliyochangamana kiasi, yenye kuzungumzia tajriba ya maisha ya binadamu kwa ubunifu.  Kwa mujibu wa Wamitila (20...