RIWAYA YA KISWAHILI NA TAHAKIKI
RIWAYA YA KISWAHILI NA TAHAKIKI CHUO KIKUU CHA ARUSHA NA: LEBABU S.S Maana ya Fasihi Dhana ya fasihi imekuwa ikijadiliwa kwa karne nyingi na wataalamu mbalimbali ulimwenguni kote. Huko Ulaya dhana hii ilikuwa ikihusishwa na vitu kadhaa. Hata Afrika neno fasihi limezua mjadala mkubwa sana kwa wanafasihi katika taaluma hii. Miongoni mwa wataalamu ambao wamechangia kuhusu maana ya fasihi ni pamoja na Sengo na Kiango (1977), Kirumbi (1975), Mazrui (1980) na wengine wengi. Kiulimwengu hasa huko Ulaya dhana ya fasihi imekuwa ikihusishwa na neno la kilatini litera likiwa na maana ya herufi au uandikaji. Hata neno la Kiingereza ‘literature’ limechipuka kutoka hapo. Mitazamo iliyotawala dhana ya fasihi ipo mitano Mtazamo wa kwanza ni ule unaodai kuwa fasihi ni tafsiri ya neno la Kiingereza Litereture ambalo asili yake ni neno la Kilatini likiwa na maana ya herufi au uandikaji. Hivyo basi mtazamo huu unaamini kuwa fasihi ni jumla ya maaandishi yote katika lugha. Wellek ...